Mchungaji Jesse Jonathan na Bi. Mch. Happiness Jesse Jonathan ni Viongozi na Waanzilishi wa Christ Revival Church (CRC) International. Maono ya Kanisa la Christ Revival Church International ni “ Kuhubiri Injili ya Kristo ili Iwaokoe watu kutoka ufalme wa giza wa shetani, Iwafungue waliofungwa na kuinua kizazi cha watumishi wa Mungu wanaotembea katika Ushuhuda wa Neno la Mungu. Pia kuleta uamsho katika mwili wa Kristo na suluhisho katika kubadilisha maisha , yatakayopelekea kubadilisha Taifa na hatimaye Dunia kwa kuwaimarisha watu wa Mungu kupitia maombi, sifa na kuabudu.