in the future - u will be able to do some more stuff here,,,!! like pat catgirl- i mean um yeah... for now u can only see others's posts :c
Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemshauri Rais wa sasa wa nchi hiyo, William Ruto, kuwa mamlaka aliyo nayo sasa ni ya kupita, hivyo afanye kazi yake ya kuendesha nchi hyo na kuifanyia kila lililo bora, hata kama yeye hakumuunga mkono wakati anagombea, kwani yeye alijitahidi katika kipindi chake na alikabidhi madaraka hayo kipindi chake kilipomalizika.
7 - 2
Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo Mubyazi akiongoza Jopo la wataalamu wa Mitandao na Teknolojia ya Habari kutoa mafunzo juu ya namna ya kutunza siri katika vifaa vya kisasa vya mawasiliano hususani Simu na Tarakilishi Mpakato (Laptop) wakati wa Mkutano wa Wakurugenzi wa Mawasiliano wa Majimbo Katoliki na Taasisi za Kanisa Katoliki, makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini Dar es salaam.
#FreedomOfSpeech #Cybersecurity #trending
4 - 0
Baadhi ya Picha za siku ya pili ya Mkutano wa Wakurugenzi wa Mawasiliano wa Majimbo Katoliki na Taasisi za Kanisa Katoliki nchini waliokutana kujadili mambo mbalimbali huku pia wakipata Mafunzo juu ya Utunzaji wa Usiri katika vifaa vya kisasa vya Mawasiliano ikiwemo simu na Tarakirishi mpakato kutoka kwa Wataalamu wa Tehama kutoka Taasisi ya Jamii Forum.
Katika Mafunzo hayo pia Askofu Mwenyekiti wa Mawasiliano ndani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Mhashamu Euzebius Nzigilwa alihudhuria na kushiriki kikamilifu.
#kanisakatolikitanzania #jamiiforums #katoliki #ikulu #ITVUpdates #cybersecurity
5 - 0
MAMA MZAZI WA RAIS MSTAAFU UHURU KENYATTA AONDOLEWA ULINZI
-
Hatua inakuja ikiwa ni siku moja tangu Serikali iondoe walinzi wa Raila Odinga na viongozi wengine wa Upinzani zaidi ya 50 wakati Serikali ikiwa kwenye shinikizo la Maandamano yaliyoitishwa na Odinga
-
Awali Mama Ngina ambaye ni Mke wa Rais wa zamani alikuwa na Walinzi 30 na baadaye wakapunguzwa hadi 8 baada ya William Ruto kuingia Madarakani. Taarifa zinaeleza kuwa hajajulishwa chochote kuhusu uamuzi huo wa Serikali
-
Ikumbukwe mara kadhaa Rais Ruto amekuwa akimtuhumu Uhuru Kenyatta kufadhiliu harakati na kushirikiana na Upinzani akiwemo Raila Odinga kwa lengo kuvuruga utawala wake.
-
#JamiiForums #Governance #HumanRights #Accountability
3 - 0
SERIKALI YAAGIZA SHULE ZIFUNGWE NAIROBI NA MOMBASA KUEPUKA VURUGU ZA MAANDAMANO
-
Mawaziri wa Elimu na Mambo ya Ndani wametoa agizo hilo litakalozihusu Shule za Sekondari na Msingi zinazodaiwa kulengwa na Waandamanaji kwaajili ya kusababisha vurugu katika Maandamano ya Julai 19, 2023
-
Taarifa ya Serikali inasema "Kama hatua ya tahadhari ya kuhakikisha usalama wa Watoto, ni amri kuwa Shule za Msingi na Sekondari katika miji ya Nairobi na Mombasa zifungwe, Wizara ya Elimu itatangaza muda wa kurejea baada ya tathmini ya Usalama"
-
Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga na ametangaza kufanya kile alichokiita Maandamano ya Kimapinduzi kuanzia Julai 19 hadi 21, 2023 na Siku zote za Jumatano, Alhamisi na Ijumaa za kila Wiki.
-
#JamiiForums #Governance #HumanRights #Accountability
4 - 1
ZANZIBAR: AFANDE RAMA AACHIWA HURU, AANGUA KILIO MAHAKAMANI
-
Mahakama ya Mkoa wa Vuga Mjini Unguja imemuachi huru Ramadha Ali (Afande Rama) aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la kuruhusu kuingiliwa kinyume cha maumbile
-
Hakimu Khamis Ali Simai amesema mshtakiwa hana hatia kutokana na ushahidi kutotosha kumtia hatiani, hivyo amemuachia huru, uamuzi ambao ulimfanya Rama aanze kulia huku akitoka Mahakama kwenda kwenye gari la ndugu zake kisha kuondoka bila kuzungumza chochote
-
Jumla ya mashahidi 9 waliwasilisha ushahidi wao ambao haukuweza kutosha kumtia hatiani Rama ambaye ni mtumishi wa Jeshi la Polisi
-
#JFMatukio #JamiiForums
1 - 1
50% ya ujenzi wa shule mpya haukukamilika licha ya fedha zilizotengwa kutumika zote
-
Ripoti ya #CAG ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 2021/22 inaonesha ujenzi wa shule mpya za Sekondari 59 sawa na 50% ya shule zilizotengewa fedha za #UVIKO19 hazikuwa zimekamilika licha ya kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo kuwa zimetumika zote
-
Changamoto hizi katika ujenzi wa miradi ya elimu kwenye baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zimesababisha mapungufu kwenye miradi ya elimu katika Shule za Msingi na Sekondari
-
#HudumaKwaJamii #JFUwajibikaji23 #JFHuduma #RipotiYaUwajibikaji23 #JamiiForums
4 - 0
Ukaguzi wa #CAG 2021/22 ulibaini changamoto za Ufanisi kwa Taasisi za Usimamizi ambapo Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lilinunua Mita za Umeme 874,019 zenye thamani ya Tsh. Bilioni 115, bila mita hizo kuthibitishwa na Wakala wa Vipimo
-
Kanuni ya 22 (1) ya Kanuni za Uzani na Vipimo za mwaka 2019 zinaelekeza kuwa hakuna mita itakayoruhusiwa kutumiwa na mkandarasi au mnunuzi yeyote kwa madhumuni ya kupima umeme au gesi inayotolewa au kutumika kwake isipokuwa imethibitishwa
-
Mita ambazo hazijathibitishwa na Wakala wa Vipimo zinaweza kuleta au kusababisha hasara kwa watumiaji wa umeme au Shirika la #TANESCO
-
#JamiiForums #JFUwajibikaji23 #UsimamiziTaasisi #UwajibikajiTaasisiZaUmma #RipotiYaUwajibikaji
#JFHuduma
3 - 0
JAMIIFORUMS YATWAA TUZO 2 ZA KIDIGITALI TANZANIA
Tuzo ya kwanza ni ya Taasisi Bora inayohamasisha na kutetea Haki za Kijamii na Kisiasa Mtandaoni na Tuzo ya 2 ni ya Kiongozi Bora wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayofanya Uchechemuzi wa Masuala ya Uwajibikaji na Haki za Kidigitali
JamiiForums inatoa shukrani kwa Waandaaji wa Tanzania Digital Awards (TDA) kwa tuzo hizi pamoja na kutambua mchango wetu katika kuhamasisha Haki za Kijamii na Kidigitali
#JamiiForums #JFDigitali #TDA2023
3 - 0
KENYA: WATANZANIA WAKAMATWA WAKIELEKEA SOMALIA KUJIUNGA NA AL SHABAAB
-
Polisi nchini humo wanawashikilia Abdirahman Shaffi Mkwatili, (25) na Sadam Jafari Kitia, (30) waliokiri walikuwa wakielekea kujiunga na #AlShabaab, baada ya kuwakamata Julai 12, 2023 wakiwa na daftari lililoandikwa kwa Kiswahili ambalo linadaiwa walikuwa wakitumia kuwaongoza kutoka #Tanzania hadi Jilib, #Somalia
-
Kukamatwa kwao kumekuja Wiki 2 baada ya Watanzania wengine watatu, Abdul Saif Salimu, Zuberi Ngare Mtondoo na Seif Abdalla Juma, waliodaiwa kuwa katika harakati za kujiunga na kundi hilo kukamatwa nchini humo kufuatia taarifa za Wananchi
-
Polisi wamedai kubaini kuwa mtindo wa daftari hutumika na raia wanaosafiri kujiunga na Al Shabaab, baada ya kusajiliwa na kuwezeshwa na wahudumu wao wa #Tanzania, ili kukwepa mawasiliano wanapokuwa njiani au kuwauliza watu ili kuepusha kuibua wasi wasi
-
#JamiiForums #Diplomacy
5 - 3
JamiiForums is Tanzania’s most visited and trusted website and the most popular destination for Kiswahili speakers in East Africa and around the world that emphasizes the use of user-generated content for reporting critical issues.